Na Mwandishi wetu.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere ametembelea kijiji cha Msomera kwa lengo la kuangalia ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayojengwa na Serikali katika kijiji hicho.
Katika ziara hiyo CAG Kichere amekagua nyumba 1,500 ambazo tayari zimekamilika kwa ajili ya Wananchi wanaotokea Ngorongoro kuhamia kijiji cha msomera kwa hiari sambamba na kukagua miradi ya barabara, maji, shule na huduma za afya, umeme na maeneo ya mifugo kama minada na malisho.
Mkuu wa wilaya ya Handeni mhe. Salum Nyamwese ameipongeza serikali kutokana na jitihada kubwa za uwekezaji katika kijiji hicho ambacho kimekuwa cha mfano Tanzania.
Katika ziara hiyo Bw. Kichere alifuatana na Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro bwana Abdul-Razaq Badru pamoja na watendaji wengine wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.