Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi katika uwanja wa CCM mjini Ngudu Wilayani Kwimba, alipopita kuwasalimia wakati akianza rasmi kampeni leo Agosti 29, 2025 jijini Mwanza. Pamoja na kuwahutubia wananchi pia alimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kwimba ndugu Bulala Mutesigwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sumve Bujaga Charles na madiwani wa chama hicho.