Mgombea mwenza wa kiti cha Urais Emmanuel Nchimbi akizungumza jijini Mwanza

………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuel Nchimbi amezindua Kampeni Mkoani Mwanza ambapo ameeza mambo saba yatakayotekelezwa mkoai humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Nchimbi amezindua kampeni Leo Ijumaa Agosti 29, 2025 katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Amesema Katika miaka mitano ijayo wataboresha uwanja wa ndege wa Mwanza ili uweze kuwa na sifa ya Kitaifa mbali na hilo amesema watakamilisha ujenzi wa Reli kutoka Mwanza hadi Isaka sanjari na ujenzi wa Meli mbili.
“Tutahakikisha tunasimamia miradi hiyo vizuri ili iweze kutekelezwa kwa wakati na iweze kuleta tija kwa wananchi wa mkoa wa mwanza”
Aidha, amesema miradi mipya 76 ya maji itaanzishwa ili kuhakikisha wanamaliza changamoto ya maji mkoani humo.
Pia amesema Serikali itajenga nyumba ambazo zitapangishwa kwa gharama nafuu ili kuwapunguzia wananchi gharama za maisha.
Nchimbi ameeleza kuwa watarasimisha shuguli ndogondogo za wafanyabishara hataua itakayowasaidia kukopesheka kwa uraisi.
Ameongeza kuwa wataboresha ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ili kuboresha ajira kwa vijana mkoani humo.