

Klabu ya Simba SC imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa Taifa Stars na JKT Tanzania, Wilson Nangu, kwa mkataba wa miaka miwili, na hivyo kumwondoa rasmi kwenye rada za watani wao wa jadi, Yanga SC.
Nangu amekuwa mhimili muhimu wa safu ya ulinzi ya JKT Tanzania, jambo lililomvutia Simba SC kuisaka saini yake kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, JKT Tanzania imekubali kumuachia Nangu kwa sharti la kupewa wachezaji David Kameta na Awesu Awesu kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Mbali na Nangu, inadaiwa Simba pia imemalizana na Yakoub Seleman, kipa namba moja wa JKT Tanzania na Taifa Stars aliyecheza mashindano ya CHAN 2024, ambaye tayari ameshaagwa na klabu yake hiyo.
Simba SC hivi karibuni imerejea nchini kutoka kambi ya maandalizi nchini Misri, ikiwa tayari kwa mechi za Ligi Kuu zitakazoanza Septemba 17, 2025. Aidha, mashabiki wa klabu hiyo wanatarajia kushuhudia Simba Day mnamo Septemba 10, 2025, ambapo Simba itapambana na Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.