NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
CHAMA Cha Wanadishaji Tanzania TACA kimeiomba serikali kufanyia maboresho Sheria inayowaongoza kwa lengo la kusaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Ombi hilo limetolewa leo Agosti 30,2025 Jijini Dar es salaam katika Mkutano wa 3 wa mwaka wa TACA ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Phidel Katundu ametaja kuwa moja ya changamoto inayowakabili ni jamii kutokuwa na elimu kuhusu majukumu yao ya udalali na unadimishaji jambo linalohatarisha usalama wao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao
“Umma wa watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusu mnadimishaji na dalali ni watu wa namna gani ukienda kwenye jamii unachukuliwa tofauti na tafsiri ya watu waliyonayo kichwani ukienda inabidi kutoa elimu ili kuwa salama”Katundu amesema.
Katundu ameeleza kuwa Muingiliano wa mamlaka nyingine inapotokea kunadimisha baadhi ya Mali za wadaiwa imekuwa shubiri kwani baadhi yao wamekuwa wakikimbila mahakamani kuzuia Mali walizoweka kuombea mkopo ili zisiuzwe jambo ambalo linakwamisha utekelezaji wa kazi yao.
Hata hivyo,Katundu amebainisha kuwa wamewasilisha ombi serikalini kuomba chama hicho kipewe nguvu za kimamlaka ili kiweze kusimamia wanachama wake na kulipa chama hicho nguvu.
Mbali na hayo Katundu ametoa wito kwa madalali ambao hawajajiunga na chama hicho kujiunga ili kujenga umoja wenyenguvu kwa lengo la kusaidiana pale inapotekea changamoto.
Vilevile,Mjumbe wa Kamati kuu ya madalali Bw. Chuki Shaban amesema kupitia Mkutano huo wamezibaini changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili kutokana na kutofanyiwa maboresho ya Sheria ambayo ilikua ikitumika tangu mwaka 1928.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanfin Consultant Bw.Idani Bangula amesema kupitia Mkutano huo wamebaini iko haja ya mabadiliko ya shughuli za unadishaji wa maadili kutokana na kubaini Sheria ya unadishaji wa mali iliyokuwepo haiendani na wakati wa sasa.
Naye,Afisa Mwandamizi wa Usimamizi Mali za serikali( Wizara ya fedha)Bi.Karerema Kwale amesema wamepokea changamoto mbalimbali ambazo madalali na waendesha minada wanazokutana nazo kwenye shughuli zao za Kila siku hivyo ameahidi kwenda kuzifanyia kazi
Hata hivyo,Karerema ametoa rai kwa kwa wadau wanaofanya kazi za minada na udalali kupata leseni ya kufanya shughuli hizo kwani ni tasnia rasmi inayoipatia serikali Mapato na kufanya kazi hizo bila kufuata taratibu ni ukikajj wa matakwa ya kisheria.