Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kiloleli Jacob Mutashi
………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wagombea wa vyama vyote vya siasa waliokubali kushiriki uchaguzi wametakiwa kufanya kampeni za kistaarabu ili kuilinda Tunu ya amani iliyowekwa na Mwenyezi Mungu.
Hayo yamebainishwa na Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kiloleli Jijini Mwanza, Jacob Mutashi alipokuwa akizungumza na Fullshangwe Blog ofisini kwake.
Amesema viongozi mbalimbali watakaoiongoza nchi yetu wameanza kampeni hivyo ni wajibu wetu viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa ili zoezi la uchaguzi liweze kukamilika kwa wamani.
Amesema viongozi hawa wanaotaka kuingoza nchi yetu wajitahidi sana kuepukana na maneno ya uchochezi ambayo yataathiri ustawi wa nchi ya Tanzania.
“Wagombea wanatakiwa wafahamu kuwa katika mchakato mzima wa uchaguzi kunakupata na kukosa hivyo inapotokea umekosa mjitahidi kuridhika kwani misho wa uchaguzi huu ndio mwanzo wa uchaguzi wa 2030”,
Aidha, amewaomba wananchi kujitokeza kwaajili ya kusikiliza sera za wagombea ili uchaguzi unapofika waweze kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo.