
Gairo, Morogoro – 30 Agosti 2025 – Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amepokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi wa Gairo, mkoani Morogoro, akiwa njiani kuelekea Kibaigwa, Dodoma kuendelea na mikutano ya kampeni.
Wananchi wa Gairo walijitokeza kwa wingi barabarani na kwenye viwanja, wakimshangilia kwa nyimbo, mabango na salamu za upendo. Wameahidi kumpa kura nyingi za “Ndiyo” ifikapo Oktoba 29, 2025, wakisisitiza imani yao kwa uongozi wake unaoendelea kuwaletea maendeleo.
Dkt. Samia aliwashukuru WanaGairo kwa mapokezi hayo ya heshima, akiahidi kuendelea kusikiliza na kushughulikia kero zao kupitia sera na ilani ya CCM inayolenga kuboresha maisha ya kila Mtanzania.