Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na katika ziara hiyo ametembelea chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.
Wakati wa ziara hiyo Mhe. Mohadi amekutana na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaopatiwa mafunzo ya uongozi katika chuo hicho yanayolenga kuwajengea uwezo viongozi, ambapo amepongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka programu za kuwajengea uwezo viongozi wao.
Mafunzo hayo ya Uongozi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa yameanza tarehe 29 Agosti hadi 04 Septemba, 2025 na yanaratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi (UONGOZI INSTITUTE).