
Afisa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Bw. Goodluck Assenga akitoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wakazi wa Manispaa ya Temeke walioshiriki katika Kongamano la Nishati Safi lililofanyika Agosti 30, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kibasila, jijini Dar es Salaam.


Mgeni rasmi wa Kongamano la Nishati Safi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN), Mhe. Janeth Mbene (kulia) akipewa elimu ya matumizi ya majiko yanayotumia nishati ndogo ya umeme.




Afisa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Bw. Goodluck Assenga akitoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa vikundi vya wajasiliamali wa Manispaa ya Temeke walioshiriki katika Kongamano la Nishati Safi lililofanyika Agosti 30, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kibasila, jijini Dar es Salaam.

Maafisa Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi wa Kongamano la Nishati Safi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN), Mhe. Janeth Mbene (katikati).




………………
Na Goodluck Assenga, Dar es Salaam
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limeshiriki Kongamano la Nishati Safi lililoandaliwa na Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania kwa kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wajasiriamali wadogo zaidi ya 70 wakiwemo Mama Ntilie, Baba Lishe na makundi mengine ya wafanyabiashara wadogo kati ya hao 20 wamejiorodhesha kupata majiko hayo.
Kongamano hili limefanyika leo Agosti 30, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Afisa Huduma kwa Wateja, Bw.Goodluck Assenga ameeleza kwamba Umeme ni nishati nafuu zaidi jikoni.
Kwa kutumia vifaa sahihi vya umeme, kwakuwa nishati hii inaokoa muda jikoni, inatunza mazingira na ni rafiki kwa mtumiaji kwa kuwa ni salama.
Aidha, wajasiriamali hao walipata kuona kwa vitendo namna majiko hayo yanavyofanya kazi kwa kupika vyakula mbalimbali kwa urahisi na haraka.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Uwezeshaji wanawake Tanzania (TAWEN) Mhe.Janeth Mbene, ambae ameipongeza TANESCO Temeke kwa juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.