Na Mwandishi Wetu,Arusha
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema kwamba kazi ya chama hicho kwa sasa ni kuisaka dola kwani mchakato wa kura za maoni zilishapita hivyo hakuna sababu ya kuwa na mgawanyiko tena.
Wsira ameyasema hayo Agosti 31,2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama hicho wakati wa kikao cha ndani ambapo ametumia kikao hicho kuelezea mchakato wa kura za maoni hadi kupatikana walioteuliwa kugombea ubunge na udiwani,
“Kazi yetu ni kuhakikisha mtu ashinde… kwahiyo muache kugawanyika kwasababu kura za maoni zimeshapita hivyo tugawanyike kwa ajili ya zile.
“Wewe unagombana na hewa maana kura zile zimeshapigwa, tena unagombana na mtokeo ambayo na wewe mwenyewe ulikuwepo wakati wa kuhesabu kura umeshuhudia halafu unamkasirikia nani? Unakasirikia matokeo au aliyetangaza, unamkasirikia nani?
“Hakuna hoja hapo bali kwa sasa hoja ni CCM kupata dola na hayo mengine yote tunayoyafanya yote ni mchakato wa kufikia lengo la kupata dola.Hivyo msipoteze lengo kwasababu ya mchakato wa ndani, huo ujumbe wangu wa leo,”amesem Wasira
Amefafanua uongozi huo na kazi ya kusema nani anakuwa na nani hawi ni kazi mbaya na ngumu na amewaambia kutokana na nguvu ya ubinadamu maana wao sio malaika na mpaka hapo walipofikia ni vema wakapongezwa maana kazi yenyewe ngumu.
“Nilikuwa namwambia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha rafiki Sabaya mbona mwanao hakuteuliwa ,nami nilikuwa na mwanangu anagombea lakini hakuteuliwa na mimi ndio Makamu Mwenyekiti…