
Leo, mamia ya wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Buchosa wamefuurika kwa shangwe kubwa kumwakilisha na kumusindikiza mgombea ubunge wa jimbo hilo, Eric Shigongo, alipokuwa akiwasili kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika kata ya Nyehunge.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM kutoka ngazi ya mkoa, ambao walishiriki kikamilifu kuhimiza mshikamano na kuunga mkono jitihada za mgombea huyo katika uchaguzi ujao. Wananchi walionesha mshikamano mkubwa na kuahidi kushirikiana kuhakikisha malengo ya chama na mgombea wake yanatimia.
Uzinduzi huu umeonesha nguvu na umahiri wa CCM katika kuandaa kampeni zake za uchaguzi wa Jimbo la Buchosa, huku wananchi wakitoa sapoti yao kwa dhati kwa mgombea wao.