


Pia, viongozi wa dini waakiwemo wa kiislamu wawaeleze waumini wao umuhimu wa kupiga kura katika uchaguzi mkuu ili wakachague viongozi watakaowaletea maendeleo, kulinda na kutunza amani ya nchi.
Hayo yalielezwa na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke, katika uzinduzi wa msimu wa Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhhamad S.A.W, yaliyofanyika jijini hapa usiku wa kuamkia leo, kitaifa yatafanyika wilayani Korogwe, Septemba 4, mwaka huu.
Alisema vyama vya siasa na wagombea Urais, ubunge na udiwani,kuelekea uchaguzi mkuu, waepuke matusi katika majukwaa ya siasa wakati wa kampeni za kuomba kura.
Sheikh Kabeke alisena wanasiasa na wagombea wanapoomba kura majukwaani wasitumie lugha ya matusi, wanadi sera na ilani za vyama vyao, wawaeleze wananchi na Watanzania watawafanyia nini.
“Siasa ni maslahi na maisha ya watu,inamfanya mtu kuwa rais, mbunge, waziri.Nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu na siku ya kuzaliwa Mtume Muhhamd S.A.W, tuwaeleze wananchi faida na umuhimu wa kupiga kura na waislamu tuwaeleze Mtume alifundisha nini,”alisema.
Sheikh Kabeke alisema wapo watu wamekuwa wakiutukana Uislamu, sasa wameibuka katika mitandao ya kijamii wakimtukana Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
“Hata Mtume Muhhamad S.A.W alitukanwa,Rais Samia kutukanwa mtandaoni ni ishara ya kufanikiwa asishituke wala kushangaa, hao wanaomtukana wanatafuta umaarufu na sifa ya kuonekana pia, anayeipinga CCM ndo mjanja lakini ukiitetea wewe ‘chawa’, CCM imeleta maendeleo unaachaje kuitetea? ”alisema.
Kiongozi huyo wa kiroho alisema mtu mwenye akili hawezi kumtukana Rais na wazazi wake,hivyo waislamu wawapuuze watu wanaowatukana viongozi wa dini na serikali, wasiwajibu kwani kunyamaza kwa mtu mjanja ndiyo majibu yenyewe.
“Tunaposema nchi hii tuiombee watu wanaleta kisokoro kwinyo (dharau au kitu cha ovyo), serikali hii imetuthamini kwa kuitambua siku ya kuzaliwa kwa Mtume,heshima na asili yake, amani iliyopo Tanzania inatokana na kumtambua Mtume Muhhamad S.A.W,”alisema.
Hivyo, aliwataka waislamu kuacha kujibizana na wanaoitukana BAKWATA na Uislamu, waendelee kumwombea Mtume na kumpambania.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Peter Begga, alisema nchi yetu haina dini ila watu wake wana dini,hivyo Sheikh Kabeke amefanya kazi ya maendeleo, pia kuwaunganisha waislamu na wasio waislamu ameitendea haki nafasi hiyo.