
Mgombea Mwenza wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwomba Luhaga Mpina kurejea kwenye chama chake cha awali, CCM, na ameahidi kuwa atampokea mwenyewe kwa mikono miwili.
Akizungumza Septemba 2, 2025 katika Jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu, Dkt. Nchimbi alisema:
“Atakayempigia simu Mpina amwambie kaka yake mkubwa alipita hapa. Mwambieni kwamba akinikosa kura atakuwa hana adabu ya Kisukuma, maana mimi nilipopita niliwaambia mimi ni kaka yake. Mwambieni pia anapotarudi arudishe kadi ya chama chake kipya na arudi CCM, na kadi hiyo nitapokea mimi mwenyewe, simtumi mtu yeyote.”
Luhaga Mpina, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kisesa kupitia CCM, alihamia ACT-Wazalendo baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM. ACT ilimteua kuwa Mgombea Urais, lakini Msajili wa Vyama vya Siasa alimzuia kugombea kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na mwanachama wa chama hicho, Monalisa Ndala, akidai Mpina hajatimiza vigezo vya kisheria. Kesi hiyo kwa sasa ipo Mahakamani.