
Jina langu ni Aisha, nina umri wa miaka 23. Kwa bahati au majaliwa, nimejikuta kwenye mahusiano na mwanaume Amani, mwenye umri wa miaka 43. Amani ana nafasi kubwa kitaifa, lakini kazi zake nyingi zipo nje ya nchi.
Kwa upande wa maisha, Amani amekuwa msaada mkubwa kwangu. Amenipa mtaji wa shilingi milioni kumi, na kila huduma ninayohitaji, ananiwezesha. Kwa mwezi pekee, hutumia si chini ya milioni 1.5 kwa ajili yangu.
Hata hivyo, changamoto iliyoibuka ni kwamba, baada ya muda, nimekuja kugundua kuwa Amani tayari ana mke.
Mke wake anaishi hapa Dar es Salaam. Nilipogundua hilo, moyo wangu uliniuma sana, nikamwambia tuachane.