Na Diana Deus ,Missenyi,
Shirika la hifadhi Za Taifa TANAPA kwa kushirikiana na wadau wengine wa Wanyamapori TAWIRI na TAWA wamefanya juhudi za Makusudi za kuhamisha Tembo zaidi ya 500 waliolowea katika mashamba ya wawekezaji na mashamba ya wakulima katika vijiji vya Karagwe na Kyerwa na kuwarudisha katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato.
Serikali ya mkoani wa Kagera imezindua oparasheni hiyo maalum ya kuwaondoa tembo zaidi ya 500 waliovamia makazi ya watu kwenye wilaya za Karagwe, Kyerwa na Missenyi na kuathiri mashamba Ya miwa ya Kagera Sukari ili kurudisha amani kwa jamii ambayo imesitisha shughuli za uzalishaji
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwasa ameshiriki zoezi Hilo moja kwa moja katika mashamba ya wawekezaji wa kiwanda Cha Kagera Sukari eneo la kitengule Moja ya eneo lililoathiriwa na tembo hao ambapo amesema kuwa serikali inawaondoa tembo hao ili kuwahakikishia usalama wananchi.
“Tumekuwa tukipokea malalamiko makubwa sana kutoka kwa wakulima na baadhi ya vitongoji kwa maeneo yaliyovamiwa na Tembo shughuli zimeanza kufutika bna wanachi wameama serikali yetu ni sikivu na tunahamini wataalamu wetu wa wanyama watatusaidia kuwahamisha Tembo na wanachi wataishi kwa amani .
Kamishina msaidizi wa uhifadhi Hifadhi ya Ibanda Kyerwa Dr Frederick Mafuru amewahakikishia wananchi kuwa tembo hao watahamishwa kwa amani pasipo kusababisha madhara yeyote kwa binadamu
Alisema kuwa makundi ya Tembo waliopo kwa sasa yameanza kuingia katika eneo Hilo miaka 18 iliyopita na Kasi ya kuzaliana imekuwa ni kubwa na sasa Jitihada za kuwahamisha zimeanza kuonekana baada ya kuwavalisha vinasa mawimbi vinavyowatambulisha sehemu wanapotokea na kuingia
“Tunatarajia kufanya zoezi Hilo kwa weledi mkubwa sana , jitihada za muda mfupi zimekuwa zikifanyika za kuwahamisha lakini Bado hazikuzaa matunda ya kudumu na sasa tumepata kifaa maalumu kitakachosaidia kuwahamisha moja moja ili wasiendelee kuleta madhara kwa Wananchi ,mashirika yetu ya hifadhi za Taifa na mashirika ya Wanyamapori tutafanya kazi hii kwa weledi mkubwa na haraka ili kurejesha amani “alisema Mafuru
Alisema hifadhi ya Taifa ya Burigi chato imetenga eneo la kutosha Kwa ajili ya kuhamishia Tembo hao ili kuendeleza utalii wa Tembo ambao utawavutia maelefu ya wageni kufika katika hifadhi hiyo ambapo alisema kuwa Eneo Hilo litakuwa na malisho ya kutosha pamoja na maji ya kunywa na sehemu salama ya Tembo
Akitaja athari zilizojitokeza katika eneo la kitengure Baada ya ongezeko la Tembo hao ni Ujangili wa kuwaua kuongezeka, Uchumi wa kuzalisha Sukari Kushuka ,vifo kwa wanachi pamoja na shughuli za uzalishaji katika vijiji vilivyovamiwa na Tembo kufungwa.
Lebahath Emmanuel meneja kilimo kutoka kiwanda cha Kagera Sukari alisema kuwa Hekta 183 za mashamba ya miwa zimeharibiwa zenye uzito wa miwa tani laki 2 ambazo zingezalisha Sukari ya shilingi bilioni 6
Alisema pia nje ya changamoto ya mashamba ya miwa kuharibiwa wafanyakazi na vibarua wameacha kazi kwa hofu ya kuuliwa na Tembo na makazi yao kuharibiwa.
Kwa niaba ya wakazi walioathiriwa na tembo hao Jacksos Cosmas wenyekiti wa kijiji Nyakashenye kata ya Businde Wilayani Kyerwa alisema kuwa Viongoji vingi vimefutwa kutokana na Athari za Tembo na wananchi wamehama makazi yao Na kukimbilia pasikojulikana.
Alitoa shukurani kwa kuendelea Kubaini kilio Chao kwa muda mrefu na kudai kuwa kama Tembo hawatarudi wananchi watafanya shughuli zao za ushalishaji na kuendelea na kilimo Cha mazao .