NA JOHN BUKUKU- RUNGWE
CHIFU msaidizi wa Mtokela Kata ya Ndoto wilayani Rungwe Oscar Msafiri Mwakatungila mkazi wa Mtokyela amesema kuwa wao wanaamini zaidi katika amani viongozi wetu wa chama cha mapinduzi wametusaidia kudumisha amani mpaka hapa tulipo .
Amesema kuwa , ameona vituo vya afya kila kata ambavyo kabla ya hapo havikuwepo na amefanya miradi mingi mipya ambayo imeendelea.
“Tunashukuru Mungu japo ilikuwa ni mwanzo sasa tunataka tumpe mitano mingine ili atusaidie kwenye barabara na vitu mbalimbali ambavyo bado vimesalia hivyo tukimpa mitano tena atafanya yale ambayo yamesalia.”
“Sisi kama viongozi wa kimila ndio ambao tulianza kabla ya mkoloni tulikuwepo na baada ya mkoloni tupo na sasa serikali ipo na hivyo tunahitaji ushirikiano mkubwa na serikali kwani serikali inapotuacha nyuma sisi ndio tunaojua mipaka na vyanzo vyote vya mapato kwenye miji yetu.”amesema .
Aidha amesema ameiomba serikali iwape nafasi kwenye upande wa ardhi mazingira maliasili na wawe wanashirikishwa kwa ulinzi kwani wao ndo wanaoelewa hapa kwa nani hapa kwa nani .
“Ushirikiano wetu na kiongozi wa machifu Chifu Angaya ni mzuri sana kwani ametuonyesha nafasi kuwa na sisi tupo tunahitaji hii nguvu iongezeke zaidi kwani kuna sehemu zingine chifu hatambuliki kama na yeye ni kiongozi.”amesema.