Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Makambako
YAANI ni full vibe… ni shangwe tu kwa wananchi wa Makambako!Ndivyo unavyoweza kueleza wakati mamia ya wananchi wakiwa wamejitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan
Katika mkutano huo ambao unafanyika mapema asubuhi ya leo Septemba 6,2025 wakimsubiri mgombea Urais kupitia CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wamekuwa na Vibe(shangwe) la kutosha.
Vibe la wananchi Katika mkutano ya Dk.Samia kwa sehemu kubwa inatokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya 2020-2025 ambayo imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 100.
Pia, vibe la wananchi kote ambako Rais Samia anapita linatokana na miradi mikubwa ambayo imetekelezwa katika miaka minne na nusu ya uongozi wa Dk.Samia anayetumia falsafa ya 4R.
Kwa Makambako mkoani Njombe baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kuanzia saa 12 asubuhi kumsubiri Dk.Samia Suluhu Hassan wamesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia imefanya mambo makubwa ya maendeleo.
“Sisi Makambako wote tumeamua katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu tunasubiri ifike Oktoba 29 twende kutiki kwa Dk.Samia lakini tunakwenda kutiki kwa mgombea ubunge wetu Daniel Chongolo.”