*Awaambia anayedharau mwiba mguu huota tende… hivyo lazıma aombe kura
*Asema yaliyofanywa na Serikali ya CCM ndio sababu ya mikutano yake kujaza watu
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewajibu wanaojadili kwanini CCM na mgombea wake anatumia nguvu kufanya kampeni wakati upinzani haupo.
Majibu ya Dk.Samia kuhusu wanaojadili kwanini CCM na mgombea wake wanatumia nguvu wakati hakuna upinzani ameyatoa alipokuwa akizungumza na maelfu ya wananchi wa Mlowa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma baada ya kusimama kuwasalimia na kuwaomba kura alipokuwa mkoani Iringa.
“Niseme jambo moja dogo,wanajadili kwanini CCM mama (Rais Samia)anatumia nguvu sana wakati upinzani haupo? Waswahili wanasema anayedharau mwiba mkimchoma mguu unaota tende.
“Sasa usisubiri mpaka uchomwe na msumari…hapana hata mwiba lazima ushughulikie, kwahiyo kama misumari imelala au ipo iliyochomoza ama iliyosimama lazima tuishughulikie ipasavyo ndio maana nimekuja kuomba kura.
“Pia wana CCM wameridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika na ndio maana kila tunakokanyaga hakuna umma bali kuna utitiri ,watu ni wengi kwasababu wameridhishwa na kazi iliyofanywa na Serikali ya Cha Mapinduzi.
“Na hilo ndilo jawabu kubwa zaidi kuliko yote.Hivyo ndugu zangu nimesimama hapa kuomba kura nikiwa sina wasiwasi kabisa na Mkoa wa Dodoma.Lakini uungwana unapokuwa na haja ni kwenda kwa mwenzio ukamuomba kwa heshima.
“Kwahiyo na mimi kwa heshima na taadhima wana Mvumi nimesimama hapa kuomba kura,nikimuombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mimi niliyesimama hapa,lakini wabunge na madiwani. Hivyo naomba kura kwa maeneo matatu.”
Awali wakati anazungumza na wananchi hao, Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema ratiba yake ilikuwa ya kupita awasalimie na Mlowa yeye ni nyumbani kwasababu ni sehemu ya Chamwino
“Kwahiyo nikaona si heshima nipite tu bila kusimama hivyo nimesimama tusalimiane.Nawashukuru sana wa Mlowo, wana Mvumi na wana Chamwino kwa kujitokeza kwa wingi namna hii.
“Tumesimama kuomba kura, niwaombe kura kwa chama cha Mapinduzi, niombe kura kwa makundi matatu Rais,Wabunge na madiwani. Naniajiamini kusimama kuomba kura kwasababu kazi zilizofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi zinaonekana.Tumetekeleza miradi mingi yenye kugusa maisha ya wananchi.”
Amesisitiza Chama cha Mapinduzi na Serikali yake inasema na inatekeleza hivyo amesema wakipata ya wananchi ili kuongoza Serikali katika miaka mitano ijayo watafanya makubwa zaidi huku akiweka wazi yajayo yanafurahisha
Aidha amesema yeye ni mama hivyo ataendelea kuwa mlezi kwa watoto wake.”Kwahiyo nami najua nina watoto wa kulea wakiwa na maslahi yao lazima niyazingatie.