Leo, tarehe 8 Septemba 2025, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Migiro amemfikishia Dkt. Mwinyi salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mgombea wa Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Dkt. Migiro amempongeza Dkt. Mwinyi kwa kuaminiwa tena na kuteuliwa na Chama kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar.