Na Mwandishi Wetu,Mkurunga
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mary Chatanda amesema Chama hicho kimewateua wagombea wanaokubalika kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Hivyo amesema jukumu kubwa la wananchi ni kuhakikisha wanawachagua wagombea wa Chama hicho kuanzia nafasi ya Urais ,wabunge na madiwani kwa kuwapa kura nyingi za ndio ifikapo otoba 29,mwaka huu
Chatanda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Mkurunga ambapo yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi ambapo amesema katika kipindi cha uongozi wa Dkt .Samia Suluhu Hassan ameweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.
Kuhusu kampeni Chatanda amesema mkoa wa Pwani kupitia wabunge waliokuwepo katika Mkoa huo wamefanya kazi nzuri na wengi wao wameweza kuteuliwa kuwa mawaziri kutokana na uchapakazi wao .
Aidha amewaomba wananchi kumpa kura nyinyi mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia kwani wakimpa miaka mingine mitano atakwenda kufungua fursa za uwekezaji na hivyo kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa Mkuranga.
Ametumia nafasi hiyo pia kuzungumzia taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii ambapo amewaomba wananchi kuwaachana nazo na kuhakikisha wanamchagua Dkt Samia kwa kishindo ili vituo vya afya,zahati ,na maeneo mengine yanaendelea kuboreshwa.
Kuhusu Ulega amewaomba wananchi kuhakikisha wanamchagua mgombea ubunge huyo. “Ndugu zangu niwaombe tukamchague Ulega na tayari mlishafanya kazi kubwa kupitia kura za maoni na Chama kimemteua Ulega kugombea Jimbo hili, hivyo hakikisheni mnakuwa naye kwenye kampeni zake kote atakakopita.”amesema Chatanda
Pia amemshukuru Mwenyekiti Chatanda kwa kumteua kwenda kuwaombea kura wagombea wa CCM huku akitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanampigia kura Dkt.Samia ,Mgombea ubunge Abdallah Ulega pamoja na wagombea udiwani.