
Katika kijiji kidogo kilichopo Tarime, aliishi kijana aitwaye Benedicto. Alizaliwa katika familia ya kimasikini sana, familia ambayo mara nyingi ililala njaa na kuamka bila matumaini ya kesho. Wazazi wake walikuwa wakulima wadogo wa mahindi na maharagwe, lakini kilimo chao hakikuwahi kuwaletea chochote cha maana zaidi ya chakula cha kutosheleza siku chache. Benedicto alikua akichunga ng’ombe na kondoo wa watu ili kupata pesa ndogo za kujikimu.
Moyo wa Benedicto ulikuwa na kiu ya mafanikio. Mara nyingi alipokuwa akikaa juu ya kilima, akitazama migodi ya madini inayochimbwa maeneo jirani, alijiambia: “Siku moja nami nitakuwa tajiri mkubwa, sitateseka kama sasa.” Kauli hiyo aliijirudia kila siku, na ndoto yake ikawa kama mwanga wa kumvuta mbali na maisha ya umaskini.SOMA ZAIDI