
Mgombea ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo, amepokelewa kwa hamasa kubwa na wakazi wa Kisiwa cha Kome mara baada ya kuwasili kisiwani hapo.
Ziara hiyo imefuata baada ya mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM kukamilika, ambapo Shigongo aliteuliwa tena kugombea kiti cha ubunge kwa muhula wa pili.
Akiwa kisiwani, Shigongo alisisitiza umuhimu wa kuvunja makundi yaliyokuwa yamejitokeza wakati wa kura za maoni, akiwataka wanachama na wananchi kuungana kwa mshikamano ili kuendeleza maendeleo ya jimbo hilo.