
Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda katikati ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro na Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.
Na Khadija Kalili Michuzi TV
KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Asha -Rose Mtengeti Migiro amezindua mafunzo ya Uzamili na Uzamivu kwa Viongozi ambayo yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza leo tarehe 09 Septemba 2025 ambapopia alikua mgeni rasmi amsesema kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa njia ya kubadilishana wataalamu watakaotoka nchini China na wangine watatoka hapa kwa lengo la kwenda kubadilishana uzoefu.
“Ninafuraha sana leo kwa kuzindua program hii itakayokua endelevu kati ya nchi hizi mbili rafiki yaliyoasisiwana Viongozi wetu wa Jamhuri ya Watu wa China kwa kupitia Chama Chao Cha CPC na Chama Cha Mapinduzi (CCM)” amesema Katibu Mkuu Dkt. Migiro.
“Kwa kupitia program hii tutakwenda kujifunza wenzetu wanafanya nini na kwa wakati huutumeoa tutor fursa hii kwa viongozi wakuu ambao watakuja kurithisha kizazi cha sasa na kijacho” amesisitiza Dkt.Migiro.
Awali Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Chen Minjian akizungumza wakati wa uzinduzi wa Program hiyo ametoa pongezi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Katibu Mkuu mwanamke wa kwanza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Migiro huku amempa pongezi nyingi Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa uongozi wake wenye mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.
Viongozi wengine waliohudhuria uzinduzi wa Programu hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mazengo Kayanza Peter Pinda ,Dean of the school of Global Leadership Chong Yang na Dean of Institute for financial studies Renmin University of China Wang Wen .
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Mzee Philip Mangula, Mukama , Mheshimiwa Balozi wa Afrika Kusini Naluthando Mayende Malope na wengine kutoka balozi zilizopo katika nchi sita marafiki.
Aidha Wang Wen amemsimfia na kumpa pongezi Dkt. Migiro kuwa mwanamke we kwanza kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Chama kikubwa barani Afrika.
Wakati huohuo Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu Mazengo Kayanza Peter Pinda amesema kuwa ni jambo la kujivunia kwa Vyama sita marafiki kuona Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere inaendelea kukuwa siku baada ya siku tangu ilipoanzishwa hadi sasa huku akitoa ahadi kwa wawakilishi wa CPC ambao ndiyo wadhamini wakuu kwamba wataendelea kupewa taarifa zote muhimu za Shule hiyo.
Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Profesa Marcellina Mvula Chijoriga amesema kuwa wanajivunia uzinduzi wa Programu hizo mbili ambapo wanafunzi kumi ni wa Uzamili ‘PhD ‘ huku wengine 22 wa Uzamivu ambapo washiriki wote wametoka katika Vyama Sita Marafiki vya Ukombozi Kusini Mwa Afrika .
“Tunatarajia kupata ujuzi kutoka Chuo Kikuu Cha Renmin ambacho ni kikongwe kwani kimeanzishwa 1937” amesema Profesa Chijoriga.