Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendegu amesema amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Singida kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kutoa taarifa za ukwepaji kwani wakwepaji ndio maadui wa maendelea yanayoonekana nchini.
Ameyasema hayo leo tarehe 11.09.2025 ofisini kwake alipokutana na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha aliembatana na viongozi wengine wa TRA alipotembelea ofisini kwake kwa lengo kumshukuru kwa ushirikiano anaondelea kuutoa kwa TRA katika ukusanyaji wa kodi.
Mhe. Halima amesema licha ya mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa kodi na kuweza kuvuka malengo, ofisi yake imejipanga kuhakikisha mkoa wa Singida unaendelea kupiga hatua zaidi katika ukusanyaji wa kodi ili kuingia katika mikoa mitatu bora katika kuchangia pato la taifa
“Naibu Kamishna Mkuunikuhakikishie kuwa tutapindua meza tumejipanga kuna kazi nyingi tunazifanya na sisi tuwe ktika tatu bora kwa mikoa inayochangia pato kubwa nchini”
Kwa upande wake Naibu Kamishina Mkuu Mcha amsema lengo la ziara yao mkoani Singida ni kisikiliza changamoto za walipakodi na kuwashukuru walipakodi na wadau wengine wa kodi akiwemo Mkuu wa mkoa ambae amekua akitoa ushirikiano mwema katika ukusanyaji wa kodi na kuweza kuvuka malengo.
“Lengo la ziara yetu mkoani Singida ni kusikiliza changamoto za walipokodi na kuwashukuru ili kuwatia moyo kuendelea kuwa walipakodi wazuri na kuwa mfano mzuri wa wafanyabiashara wengine”
Kwa upande wa wafanyabiashara wa waliotembelewa ambao ni Wild Flower Grains & Oil Mills Company Limited, Abeti Company Limited, Mohamed S. Dule, Global Pharma (STK) Limited wamemshukuru Kamishna Mkuu kwa kuwatembelea ili kujionea hali halisi na kusikiliza changamoto zao na kuahidi kuendelea kulipa kodi bila ya shuruti