Na Meleka Kulwa -Dodoma
Mkurugenzi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, amesema kuwa watahiniwa wanne wa mitihani ya cheti Cha utaalam wa Manunuzi na Ugavi (CPSP) wanatarajia kufikishwa kwenye Kamati ya usajili na Nidhamu kwa tuhuma za kukiuka taratibu za mitihani baada ya kubainika wakiwa na karatasi zenye maandishi ya Somo husika katika chumba Cha mitihani
Bw.Mbanyi ametoa kauli hiyo Leo Septemba 14,2025 ofisini kwake Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akisema Watahiniwa hao watafikishwa mbele ya kamati hiyo ili wapate haki yao ya kusikilizwa.
Alifafanua kuwa hatua za kinidhamu dhidi yao zitaamuliwa na kamati husika baada ya kuwapatia haki ya kujitetea
Aidha, Bw. Mbanyi ametoa wito kwa watahiniwa wote waliopata alama za kufeli, amewataka kujisajili upya kwa ajili ya mitihani ya Novemba 2025, ambapo usajili tayari umefunguliwa. Ameongeza kuwa wanafunzi vyuoni wanapaswa kujisajili ili kupata sifa stahiki, huku wazazi, wadhamini na waajiri wakihimizwa kulipia ada za mitihani ili kuwezesha watahiniwa kufanikisha masomo yao.
Vilevile, amewaonya watahiniwa kuepuka vitendo vya udanganyifu na ukiukwaji wa kanuni za mitihani, akisisitiza kuwa Bodi haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika.
Aidha,, amebainisha kuwa adhabu hizo kwa Mujibu wa kanuni ni pamoja na kufutiwa matokeo ya mitihani yote, kusimamishwa mihula mitatu ya mitihani na kupewa adhabu ya kulipa fedha au kifungo jela .
Akizungumzia udahili na matokeo ya mitihani ya 31 ya PSPTB amesema kuwa , jumla ya Watahiniwa 416 walidahiliwa katika mtihani huo, ambapo 382 walishiriki na 34 hawakufanya kutokana na sababu mbalimbali.
”Kati ya walioshiriki, 192 (sawa na 50.3%) walifaulu, 186 (sawa na 48.7%) walirudia masomo, na 4 (sawa na 1.0%) walifeli na kulazimika kuanza upya katika ngazi husika.”Amesema
Aidha, ametoa wito kwa Watahiniwa waliokosa alama za kutosha zakuwawezesha kufaulu, Bw. Godfred Mbanyi imewahimiza kujisajili na kurudia masomo kwenye mitihani ya Novemba 2025, ambapo dirisha la usajili limeshafunguliwa ” amesema
Pia, Bw. Godfred Mbanyi, amewaomba Wanafunzi waliomaliza vyuo kujisajili kwa ajili ya kufanya mitihani hio ya kitaaluma ili waweze kupata sifa stahiki
Kwa upande mwingine, amewataka wazazi na wadhamini mbalimbAli wakiwemo na waajiri kuwalipia ada ya maandalizi na za mitihani Watahiniwa wa mitihani, ambapo amesema hatua hio itaongeza chachu ya wataalamu katika fani husika.
Aidha, ametoa rai kwa Watahiniwa kujiepusha na vitendo vya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani, ameeleza kuwa Bodi haitasita kuwachukulia hatua Kali ili kuhakikisha Maadili katika tasinia ya Ununuzi na Ugavi inaenziwa na wadau wote.