Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar (INEC) Ndugu. Adam Mkina leo tarehe 15 Septemba, 2025 katika Ofisi Ndogo za Tume Jijini Dar es Salaam ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema tarehe 28 Oktoba 2025.
Uchaguzi Mkuu utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
“Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”.