Askofu wa Kanisa la Intenational Evangelism,Dkt. Eliudi Issangya akizungumza katika hafla hiyo jijini Arusha.
……………
Happy Lazaro, Arusha
Wanawake wametakiwa kutumia fursa zilizopo kwenye sekta mbali mbali hapa nchini kwa kufanya ubia wa kimkakati ili waweze kupata mafanikio.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taha Jakline Mkindi wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 25 ya idara ya wanawake Taifa katika Kanisa la Intenational Evangelism yaliyofanyika Sakila wilayani Arumeru.
Amesema kuwa,Taifa la Tanzania limebarikiwa kwa kila kitu hivyo ni vyema wanawake wakatumia fursa zilizopo kwenye sekta mbali mbali kwa ajili ya kuondokana na changamoto mbalimbali.zinazowakabili.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Intenational Evangelism,Dkt. Eliudi Issangya amesema kuwa kuna umuhimu wa wanawake na Taifa kwa ujumla kuliombea Taifa pamoja na Rais ili amani itawale.
Askofu Issagya amaesema kuwa, wanawake ni jeshi kubwa hivyo ni jukumu lao kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuiombea nchi yao amani pamoja na viongozi waliopo.
“Nawaombeni sana wamama nchi nzima muwe na roho ya maombi mtenge muda kwa ajili ya kuombea Taifa letu ili amani izidi kutawala .”amesema Askofu Issagya.
Kwa upande wake Jasmine Mtenda mema mjumbe waTaifa kwa niaba ya akina mama wa International Evangelism Tanzania amesema kuwa ,wamama ni jeshi kubwa na wana mchango mkubwa sana katika Taifa kwa ujumla huku akiwataka wakinamama wote kuhakikisha wanazitambua nafasi zao ipasavyo kuwa wao ni watu muhimu sana katika Taifa letu.
Idara ya wanawake wa kanisa hilo ilianza rasmi mwaka 2020 na idara hiyo imekutanisha wanawake wa kanisa hilo kutoka mikoa yote hapa nchini.