Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi tarehe 18 Septemba 2025, amefanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mkoani Arusha na kuitaka menejimenti ya Mamlaka hiyo kuendelea kusimamia uwajibikaji kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni.
Katika kikao chake na menejimenti ya mamlaka hiyo mara baada ya ukaguzi wa mradi wa Makumbusho ya Jiolojia na jengo la ofisi ya Makao Makuu ya Ngorongoro Dkt.Abbasi amesema jukumu la kila mtumishi wa umma liwe ni kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuleta tija kwa taifa.
“Simamieni watumishi walio chini yenu katika kusimamia uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo”,alisema Dkt.Abbasi.
Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo anayeshughulikia uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii Joas Makwati katika taarifa yake alisema kuwa mamlaka imejipanga kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo kukuza uhifadhi,utalii na maendeleo ya wananchi.