
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, inatarajiwa kuendelea leo, Alhamisi Septemba 18, 2025, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Kesi hiyo ilikuwa imeahirishwa Jumanne, Septemba 16, 2025, baada ya Mahakama kukubali ombi la upande wa mashtaka ulioomba muda zaidi kwa ajili ya kuandaa majibu ya hoja nzito zilizowasilishwa na Lissu.
Miongoni mwa hoja hizo, Lissu alipinga namna mashahidi wa upande wa mashtaka walivyohifadhiwa, akidai kuwa taarifa zao muhimu hazikufichwa ipasavyo na hivyo zikaonekana hadharani.
Leo, mawakili wa Serikali wanatarajiwa kuwasilisha majibu yao kwa hoja hizo, hatua ambayo inatarajiwa kuamua mwenendo wa kesi hii kubwa inayofuatiliwa kwa ukaribu na wananchi na wadau wa siasa nchini.
DKT SAMIA AIBUKIA ZANZIBAR – KAMPENI za URAIS CCM ZAZIDI KUPAMBA – AMWAGA SERA za MOTO…