NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bagamoyo kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Subira Mgalu ameahidi kuboresha huduma ya afya,maji na miundombinu ya barabara endapo akipewa ridhaa ya kuwaongoza wananchi.
Mgalu amebainisha kwamba katika kata zote 11 atahakikisha anaweka mikakati madhubuti ya kuboresha miundombinu ya barabara katika kiwango cha lami.
Pia Mgalu amebainisha kuwa endapo akichaguliwa ataleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya afya,elimu,maji,kuboresha ujenzi wa mifereji ya kisasa pamoja na huduma za kijamii.
Kadhalika ameahidi kusimamia suala la mradi mkubwa wa ujenzi wa bandari ambayo itaweza kusimamia kwa kiasi kikubwa kutoa fursa za ajira kwa wananchi wa Bamogamoyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) Martha Mlata ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo amewataka wanachama na wananchi wa Bagamoyo kumpa ushirikiano wa kutosha Subira kwa kumpatia kura nyingi za kishindo kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema anatambua uwezo mkubwa alionao Subira hivyo ataweza kusikiliza kero na kutatua changamoto za wananchi.
“Wana Bagamoyo mmepata mgombea ubunge mwenye uwezo mkubwa sana katika masuala mbali ya kimaendeleo na ninamtambua siku nyingi hivyo nina imani ataleta mabadiliko makubwa kwa wananchi ,”amebainisha Mwenyrkiti.
Naye Mgombea ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia (UWT) Hawa Mchafu ameomba wanachama wa CCM pamoja na wananchi kumpa kura nyingi za kishindo Rais Dkt.Samia,Subira pamoja na madiwani.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Aboubakar Mlawa amesema kwamba wamejipanga kikamilifu na wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu.
Uzinduzi rasmi wa kampeni katika Jimbo la Bagamoyo umehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama ambapo umekwenda sambamba na kuwanadi wagombea wa udiwani,Ubunge pamoja na nafasi ya Rais.