Na Muhidin Amri, Ruvuma
MANISPAA ya Songea Mkoani Ruvuma inatajwa kuwa miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi hapa nchini kutokana na kuvutia watu wengi hasa wageni wa ndani nan je ya nchi kuwekeza miradi mbalimbali ya kiuchumi na maendeleo.
Miongoni mwa miradi inayowekezwa ni pamoja na nyumba za kulala wageni(Lodge) Hotel na maeneo ya starehe kama vile Bar na kumbi za Burudani.
Miongoni mwa uwekezaji mkubwa uliofanywa ni kufunguliwa kwa Bar ya kisasa pamoja na Lodge Bora nay a kisasa inayojulikana kwa jina la TRIPLE 7 LOUNGE&RESTAURANT inayomilikiwa na kijana Mtanzania Tumaini Marunda Kira.
TRIPLE 7 LOUNGE & RESTAURANT imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki hii na imevutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Songea na Wilaya jirani za Namtumbo na Mbinga kutokana na uzuri wake.
Uwekezaji mpya wa TRIPLE 7&RESTAURANT iliyopo kata ya Msamala nyuma ya Ofisi za Kampuni ya Mtazamo unatatajwa kupunguza changamoto kubwa ya uhaba wa maeneo ya kupata chakula na malazi katika Manispaa ya Songea.
Kwa mujibu wa Afisa Biashara wa Manispaa ya Songea Andrew Mwafalo ni kwamba, mradi huo umeanzishwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kama siyo kumaliza kabisa sehemu ya za malazi na chakula kwa wageni kutoka nje ya Mkoa wa Ruvuma wanaofika katika Manispaa ya Songea.
“wageni watakaokuja wakati wa ziara Rais Samia Suluhu Hassan na Mgombea mwenza Dkt Emmanuel Nchimbi,watapata sehemu nzuri,safi na salama kwa ajili ya malazi,chakula na buradani mbalimbali zikiwemo vinywaji vya kila aina”anasema Mwafalo.
“Eneo hili kuna huduma zote muhimu kama chakula,vinywaji na malazi jambo litakalosaidia sana kuongeza wigo wa wa huduma kwa wageni na wenyeji wa Mji wetu wa Songea,ni vyema wadau tumuunge mkono ndugu yetu huyu Kira ambaye ametumia fedha nyingi kuwekeza”alisisitiza Mwafalo.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishina Msaidizi Mwandamizi(SACP)Marco Chillya amepongeza uekezaji mkubwa uliofanywa katika eneo hilo huku akisisitiza kuwa ni hatua muhimu ya kukuza uchumi wa ndani kupitia sekta ya huduma.
Kamanda Chillya amesema,atahakikisha usalama wa wageni na wateja wote watakaofika ili kupata huduma na shughuli nyingine za kibiashara katika eneo hilo muhimu la uwekezaji ili zifanyike kwa amani,utulivu na usalama.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TRIPLE 7&RESTAURANT Tumaini Kira,aliwashukuru wageni waliofika katika uzinduzi na kuwaomba waendelee kumuunga mkono ili aweze kufanisha malengo ya kuwatoa kuwahudumia wananchi hasa kwenye huduma za chakula,vinywaji na malazi.
“Nawaomba sana Watanzania wenzangu hususani wakazi wa Mkoa wetu wa Ruvuma,waje kuniunga mkono kwani wao ni watu muhimu sana kwangu na familia yangu ili niweze kufanikisha malengo niliyonayo ya kutoa huduma bora”amesema Kira.
“Wananchi wa Wilaya ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja na wageni kutoka nje ya Mkoa wa Ruvuma,wanakaribishwa kufika katika eneo hili,tumeshaanza kutoa huduma zote muhimu kwa masaa 24 bila kupumzika ili ukidhi mahitaji ya wananchi watakaofika kupata huduma zetu”amesema.