Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na waajiriwa wapya wa wizara hiyo wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa ajira mpya yaliyofanyika makao makuu ya Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 18 Sept 2025.
Naibu Katibu Mkuu Wizara Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemela akizungumza wakati wa mafunzo ya awali ya watumishi wa ajira mpya wa wizara hiyo tarehe 18 Sept 2025 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na waajiriwa wapya wa wizara hiyo wakati wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa ajira mpya yaliyofanyika makao makuu ya Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 18 Sept 2025.
Waajiriwa wapya wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika mafunzo ya awali kwa watumishi wa ajira mpya yaliyofanyika katika Makao makuu ya Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba tarehe 18 Sept 2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Prisca Lwangili akizungumza wakati wa mafunzo ya awali ya kwa waajiriwa wapya wa Wizara ya Ardhi yaliyofanyika jijini Dodoma tarehe 18 Sept 2025.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga (aliyevaa suti mstari wa mbele), Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Lucy Kabyemera (Kulia kwa katibu Mkuu) wakiwa katika picha ya pamoja na waajiwa wapya wa wizara hiyo tarehe 18 Sept 2025. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
…………
Na Munir Shemweta, WANMM
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewataka waajiriwa wapya wa Wizara hiyo kuwa wabunifu sambamba na kuwajibika ipasavyo ili kuboresha utendaji kazi katika maeneo waliyopangiwa.
Mhandisi Sanga ametoa kauli hiyo tarehe 18 Septemba 2025 wakati wa Mafunzo ya Awali kwa waajiriwa wapya 312 watakaohudumu katika kada mbalimbali.
‘’Kila mmoja wenu atafakari kufanya ubunifu kwenye eneo lake la kazi alilopangiwa, lengo hapa ni kuboresha utendaji kazi katika kutoa huduma kwenye sekta ya ardhi’’ amesema Mhandisi Sanga.
Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewaasa watumishi hao wapya kuwajibika ipasavyo kwa kuzingatia kazi iliyokusudiwa, muda na ubora wa kazi waliyopangiwa.
‘’Lazima muwajibike kikamilifu mpaka bosi wako akupende kutokana na kufanya kazi kwa ubora na kwa muda uliopangiwa, muwe sehemu ya mafanikio ya Wizara’’ amesema.
Vile vile, Mhandisi Sanga amewataka watumishi hao, kuwa na mahusiano mazuri kazini na kuacha kujitenga kwa kuwa maeneo ya kazi yanahitaji utendaji kazi wa pamoja. Aidha, amewasisitizia umuhimu wa kutunza siri za serikali wakati wote wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika maeneo ya kazi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera amewakaribisha watumishi hao wapya na kuwaeleza kuwa wamepata bahati kubwa ya kufanya kazi Wizara inayohudumia watu wote na ambapo amewataka kuzingatia haki, utu na uwajibikaji wakati wanapohudumia wananchi.
‘’Fursa mliyoipata mkaitumie kwa uadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma wakati wote wa kutekeleza majukumu yenu’’ amesema Lucy.