
Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Septemba 19, 2025, wamefanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju katika ofisi yake, Makao Makuu ya Mahakama, Dodoma.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano baina ya Mahakama na TLS katika masuala ya kisheria na maendeleo ya haki nchini.