

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kwa dhati mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo BAKWATA na wadau wote wa elimu katika kuimarisha maadili, kuendeleza maarifa na kuleta mshikamano wa kitaifa kupitia elimu.
Amesema kuwa elimu haiwezi kukamilika kama hakuna maadili kwani ndiyo yanayojenga utu, heshima na mshikamano wa kijamii. “Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu inakuza maarifa na ujuzi, sambamba na malezi yanayoimarisha tabia bora na maadili ya kizalendo kwa vijana wa Kitanzania”.
Amesema hayo Jumamosi Septemba 20, 2025 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia katika hafla ya usiku ya utoaji tuzo za elimu za mufti iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serena hotel jijini Dar es Salaam.
“Rais Dkt. Samia anawapongeza sana BAKWATA kwa juhudi kubwa mnazozifanya katika masuala yote ya maendeleo ya jamii hususan mchango wenu katika kuendeleza elimu na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia malezi ya maadili na maarifa, Serikali inathamini sana mchango wa taasisi za dini kama BAKWATA katika kuunga mkono malezi ya watoto na vijana”. Amesema Mheshimiwa Majaliwa.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limekuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya elimu nchini kwani limeanzisha na kuendesha shule, madrasa na vyuo vinavyotoa elimu bora ya dini na ya kawaida, sambamba na kujenga maadili mema kwa vijana.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tuzo za Elimu za Mufti ni jukwaa la kitaifa la kutambua na kuthamini michango ya kipekee katika elimu, ubunifu, malezi na maadili ya vijana wa Kitanzania. “Tukio hili linaakisi muonekano wa taifa lenye watu wanaojituma, wanaothamini elimu, na wanaochangia ustawi wa taifa letu bila kujali itikadi za dini au misimamo ya kisiasa.”
Amesema kuwa tuzo hizo zinatambua ubunifu, uongozi, mshikamano wa jamii na mchango wa wadau katika kuhakikisha elimu inakuwa jumuishi, bora na endelevu. Hili ni tukio linaloonesha kwa vitendo methali ya Mtume (S.A.W) isemayo: “