
WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa leo Septemba 22, 2025 amefungua maonesho ya nane ya teknolojia ya madini kwa mwaka 2025 ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.
Maonesho hayo ya Teknolojia ya Madini ambayo yalianzishwa mwaka 2018 yanalenga kuimarisha sekta ya madini nchini na kuhakikisha kuwa rasilimali madini
inawanufaisha Watanzania wote.
Maonesho hayo yamekuwa jukwaa mahsusi la Serikali, sekta binafsi, wachimbaji
wakubwa na wadogo, taasisi za kifedha, wajasiriamali na wadau mbalimbali wa maendeleo kukutana, kujadili na kubadilishana uzoefu.
kaulimbiu ya Maonesho ya Teknolojia ya
Madini kwa mwaka huu wa 2025 ni: “Ukuaji wa Sekta ya Madini ni Matokeo ya Matumizi ya Teknolojia Sahihi na Uongozi Bora/Shiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2025.”