Na Sophia Kingimali.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dk. Charles Msonde ametoa rai kwa wahandisi vijana nchini kutumia taaluma yao kujiajili na kuajili wenginie lakini kuhakikisha pia wanaweza kutumia taaluma hiyo kutatua changamoto mbalimbambali zinazolikabili Taifa.
Wito huo ameutoa leo Septemba 24,2025 Jijini Dar es salaam wakati akifunga kongamano la siku mbili la wahandisi vijana(YEF )liliangaliwa na bodi ya wakandarasi(ERB)
Amesema jukwaa hilo ni la kipekee kwani limekuwa na faida kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kwa jamii na Taifa kwa ujumla hivyo vijana wanapaswa kuzingatia ambayo wamefundishwa kwa muda huo wa siku mbili.
“Tunapohitimisha jukwaa hili tunapaswa tukumbuke mbegu mpaka iote ni lazima ioze hivyo niwasihi kutokata tamaa ukifanya kwa mara ya kwanza usipofanikiwa usikate tamaa jaribu tena mpka upate suluhisho ya unachokifanya”,Amesema Dk.Msonde.
Akizungumzia kuhusu ukuaji wa teknolojia amesema kufuatia na ukuaji wa teknolojia ni vyema kuwepo na majukwaa hayo ya mara kwa mara ili watu waweze kukutana na kubadilishana mawazo ili kuweza kupata wazo na mbinu mpya zinazozalishwa kila siku Duniani.
“Kwa mustakabali wa Dunia ya sasa hatuna budi kuwa tunakutaka mara kwa mara na tubadilishane uzoefu,na tumeona hivi karibuni tumeshuhudia kigunduzi cha vitu vya kigeni kimefungwa sehemu zinaporukia ndege hii imesaidia viwanja vyetu kuwa salama hii ni moja tu kuna bunifu nyingi zimefanyika”,Amesema.
Aidha ameongeza kuwa wahandisi hao vijana wanapaswa kutumia mifumo ya ndani katika kuendeleza bunifu zao lakini inasaidia kukua kama mtu binafsi lakini pia na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakandarasi ERB Eng.Menye Manga amesema wataendelea kutoa mafunzo hayo kwa wahandisi vijana ili waweze kuwa chanzo cha ajira kwa vijana wengine nchini.
“Bodi itqendelea kutoa mafunzo haya kwa wahandisi vijana iwe waweze kutoboa kwenye sekta ya ajira kwa kutengeneza ajira kwao wenyewe lakini kutoa ajira kwa vijana wengine”,Amesema.
Naye,Kaimu Msajili Bodi hiyo ERB Mercy Jilalala amesema wahandisi vijana walioudhulia katika kongamano hilo ni 145 ambao walikuwa ukumbini lakini wengine 84 wameshiriki mafunzo hayo kwa njia ya mtandao.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yametokana baada ya bodi kuona vijana wengi wamekuwa wakitoka chuo na kusubiri ajira hali iliyopelekea kuwa na vijana wengi ambao wamesoma na hawana ajira.
“Bodi imeona vijana wengi wamekuwa wakiona sehemu pekee baada ya kutoka shule ni kwenye ajira lakini kupitia kongamano hili tumewapa mafunzo ya kuweza kujiajili kupitia taaluma zao”,Amesema Jilala.