Rais wa Chama hicho Dokta Ezekiel Mbao wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo.


Happy Lazaro, Arusha
Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) wameiomba serikali kutimiza kilio kikubwa na cha muda mrefu cha Wauguzi na Wakunga cha kuwatengenezea muundo mpya ambao ungeanza rasmi julai 2025 .
Aidha wameiomba serikali kuanza utekelezaji kama ilivyoahidiwa kwenye mkutano mkuu wa wauguzi nchini uliofanyika mkoani Iringa mei ,2025 ili kuongeza morali ya Wauguzi na Wakunga na kuendelea kufanya kazi kwa moyo na pia kuongeza shauku ya Wauguzi kujiendeleza kitaaluma ili kuboresha zaidi ufanisi wa huduma za uuguzi na Ukunga nchini.
Hayo yamesemwa na Rais wa chama hicho Dokta Ezekiel Mbao wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha kamati tendaji kilichofanyika jijini Arusha .
Mbao amesema kuwa, hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wauguzi juu ya muundo wa maendeleo ya utumishi wa kada ya Wauguzi na Wakunga ambapo malalamiko hayo ni muundo husika yalishawasilishwa serikalini kwa nyakati tofauti kwa kuwa hauendani na maendeleo ya taaluma na mabadiliko ya huduma jambo lililodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 2013 .
Amesema kuwa, wauguzi wamekuwa wakiiomba serikali ifanye maboresho ili kuendana na mahitaji ya taaluma kwa sasa .
“Itakumbukwa mnamo mei 9 ,mwaka huu mkutano mkuu wa wauguzi uliofanyika mkoani Iringa na kuhudhuriwa na jumla ya wauguzi 1,576 kwa niaba ya serikali Deus Sangu Naibu waziri wa nchi ,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora akimwalisha waziri mwenye dhamana na kusema alisema “nanukuu,kama nilipokwisha kusema hapo mwanzo,mhe NaibunWaziri Mkuu mkoani Tanga mwaka 2024 akiwa mgenirasmi akimwakilisha mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan alilichukua jambo hili kwa uzito na akamfikishia Mhe Rais na alituagiza tulifanyie kazi kazi na tumelifanyia kazi na limekamilika kwanhiyo naomba kuwapa habari njema muundo mpya utaanza kutumika.rasmi mwaka mpya wa fedha julai 2025”.mwisho wa kunukuu.
“Lakini cha kusikitisha mpaka sasa hivi ahadi hiyo haijatimizwa kama ilivyoelezwa na mhe Naibu Waziri hivyo wauguzi wana maswali mengi magunu ni kwa nini serikali haijatimiza ahadi yale na wakati tulipewa taarifa kuwa tayari suala hilo limeshakamilika na muundo upo tayari na utaanza kutumika rasmi julai 2025 “amesema Dokta Mbao.
Amesema kuwa, kukosekana kwa taarifa kutoka serikalini juu ya suala hili,umeendelea kuzua taharuki miongoni mwa wauguzi na hivyo kupelekea ongezeko la malalamiko kwa viongozi wakidai kuwa serikali haijatimiza ahadi ambayo imekuwa ikiitoa mara kwa mara kwenye maadhimisho kama haya na viongozi tumefanya kazi kubwa ya kutuliza hali hii na pia kuzidi kufuatilia utekelezaji wa ahadi ya serikali .”
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Pendo Shayo ameiomba serikali isikie kilio.cha wauguzi na wakunga kote nchini ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao wa kila siku .
“Wengi wana muda mrefu hawajapandishwa madaraja pamoja na mishahara licha ya wengi wao kujiendeleza kitaaluma jambo ni kinyume na kanuni na taratibu za kazi.”amesema .
Kwa upande wake Katibu Mkuu TANNA ,Chacha John ametoa wito kwa serikali kutimiza ahadi hiyo kwani wauguzi na wakunga wanafanya kazi kubwa sana katika sekta ya afya .
“Wauguzi na wakunga ndo wanakuwa wa kwanza kumpokea mtu anapokuja duniani na wao pia ndio wa kwanza kumpokea mtu anapoondoka duniani ,hivyo wana kazi kubwa sana katika kuhudumia jamii hivyo ni muhimu kwa serikali katika kuhakikisha kuwa inatatua changamoto wanazokabiliana nazo.”amesema John.