
Msanii chipukizi wa muziki duniani, D4vd, amejikuta katikati ya tuhuma nzito baada ya kuripotiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15, Celeste Rivas, ambaye alipatikana amefariki ndani ya gari lililosajiliwa kwa jina lake.
Tukio hilo lilitokea Hollywood Hills, Marekani, na limeibua maswali mengi kuhusu tofauti kubwa ya umri kati ya staa huyo na marehemu. Wengi mitandaoni wameonyesha mshangao na ghadhabu, wakitaka uchunguzi wa kina kufanyika juu ya uhusiano wao na mazingira ya kifo cha Celeste.
Hata hivyo, hadi sasa mamlaka hazijamkamata D4vd, na uchunguzi wa sababu halisi za kifo bado unaendelea. Mashabiki na wadau wa muziki wanabaki na maswali mengi bila majibu.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.