NA DENIS MLOWE , IRINGA
MRATIBU wa kampeni jimbo la Iringa Mjini Salvatory Ngelela amesema kuna kila sababu za wanachi wa Kata ya Kitwiru kukipigia kura za kishindo Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu kwa Rais , wabunge na madiwani kutokana na mambo mengi waliyofanya kutokana na ilani iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika katika kata ya Kitwiru, Ngelela alisema kuwa ilani ya CCM iliyopita na waliyofanya kwa wananchi imetekelezwa kwa asilimia kubwa hivyo wanaomba ridhaa tena kwa wananchi kwa miaka 5 inayokuja ili kuendeleza pale walipoishia.
Ngelela ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya alisema kuwa yaliyoyafanywa miaka 5 iliyopita na miaka 5 inayokuja ni mazuri zaidi na ndio maana kuna baadhi wamekimbia uchaguzi kwa kuhofia wananchi watapotezea katika kuwapa kura.
Alisema kuwa CCM wanamgombea urais ambaye amefanya makubwa kitaifa kwa muda mfupi na yanaonekana kwani ilani aimeitekeleza kwa asilimia zote hivyo wananchi wajitokeze kwa uwingi kumpa kura mama Samia.
Akizungumzia mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa mjini, alisema kuwa CCM wamewapa mgombea ambaye amejitosheleza kwa kila kitu kuanzia elimu hadi ushirikiano kwa wananchi hivyo wana kila sababu ya kujivunia na kumpa kura za kishindo Fadhili Ngajilo.
Ngelela alisema kuwa Ngajilo sio mtu wa danadana ni mtu wa vitendo sio mtu wa porojo kama ambavyo baadhi ya wagombea wa vyama vingine wanaleta porojo kwenye maisha ya wananchi.
Alisema kuwa Unapokuwa kiongozi unatakiwa kuwa mfariji wa watu wa Iringa hivyo katika hili Ngajilo ni mtu sahihi kwa wana Iringa na mtu sahihi kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.
Alisisitiza kuwa usithubutu kususa chakula kwa mtu mwenye njaa kali hivyo CCM wana njaa kali ya kuleta maendeleo ya nchi na kama chama tunashindana na yoyote anayekuja mbele yetu na tunafanya kampeni ili kuomba ridhaa kwa wananchi kutokana na njaa ya maendeleo.
“Huwezi kushika nchi bila kuomba ridhaa kwa wananchi tarehe 29 wananchi watafanyaka kazi moja ya kuchaigua ccm kuongoza nchi”, Alisema
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya iringa Said Rubeya alisema kuwa ahadi ziliahidiwa katika kata ya Kitwiru zimefanyika zote na kutolea mfano shule ya msingi Uyole, sekondari Kwavava ambazo waliahidi kujenga wamefanya hivyo.
Aliongeza kuwa ahadi ya kituo cha afya Kitwiru imetekelezwa na wananchi hivi karibuni wataanza kupata huduma hivyo kama chama wamekuja tena kuahidi ya miaka 5 ambayo watawafanyia wananchi.
Alisema kuwa kama chama wameleta ilani kwenu kwa ajili ya maendeleo ya miaka mitano ambayo imemgusa zaidi mwananchi.
“Naombeni kura nyingi kwa mama na ukiangalia mama kama ameshinda ila tunahitaji kura nyingi sana kwa ajili ya mama kwani aliyofanya kwa nchi ni makubwa” Alisema
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata hiyo, Rahim Kapufi Ameomba kura kuwa diwani ili aweze kusukumia ajenda maendeleo katika kata hiyo kwenye baraza madiwani.
Alisema kuwa wananchi wampe kura Mgombea urais Dk. Samia Suluhu Hassan mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini ,Fadhil Ngajilo na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Alisema kuwa akichaguliwa kuwa diwani atahakikisha changamoto mbalimbali katika kata hiyo zinashughulikiwa ikiwemo ya ukamirishaji kituo cha afya.
Alisema kuwa akiwa diwani atahakikisha Kuwezesha uchumi kwa kina mama na vijana bila kusahau wazee kwani suala la mikopo zimeongezeka kutoka bilioni 2 hadi 9 hivyo wananchi watapata mikopo isiyoumiza.
Aliongeza kuwa atahakikisha Suala maeneo ya kurasimisha makazi tutafanya kata zima, kupima viwanja ambavyo havijapimwa ili wananchi wamiliki maeneo halali.
Kapufi aliongeza kuwa atahakikisja Barabara za mitaa zitakwenda kurekebishwa ndio itakuwa kazi ya kwanza ili ziweze kupitika.
Mgombea ubunge Iringa mjini kwa tiketi ya CCM, Fadhili Ngajilo alisema kuwa kwa upande wake amejiandaa kuwatumikia wanachi kwa ukaribu zaidi na kuondoka ile tabia ya kiongozi kuwa mbali na wananchi.
Alisema kuwa atakuwa karibu na wananchi hivyo atawafikia wananchi kwa wakati na kuhakikisha kata zima Kitwiru ibadilike ifanane na manispaa.
Alisema kuwa atahakikisha kituo cha afya kianze kazi mara baada ya kuwa mbunge na ataendelea kunisikia katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jimbo la Iringa mjini.
Alisema kuwa atahakikisha Daraja la Kitwiru linalounganisha kata jirani ya Isakalilo lianze kujengwa kwa uharaka ili kuileta karibu kata hiyo na utalii kwani itakuwa njia rahisi kupitika.
Aidha alisema kuwa katika kata ya Kitwiru kuna kero ya soko lao la mazao hivyo nitapambana kuweza kujengwa kwa soko hilo na atalibeba kwa ajili ya wananchi.
Upande wa maji Ngajilo alisema kuwa kuna sehemu hayajafika hivyo ni kazi ambayo atashughulikia kwa haraka kwa kuwaona Iruwasa pindi atakapochaguliwa.
Aidha alisema kuwa suala la mikopo kwa kina mama, vijana kujishughulisha na shughuli mbalimbali kuhakikisha na mafanikio yao na wazee msiwe na wasiwasi na watoto pia.
Ngajilo aliomba Wananchi kumpa ushiirikiano akiwa mbunge ili waharakishe maendeleo ya jimbo la Iringa na kuwaomba kura za kishindo kwa mgombea urais Dk Samia Suluhu Hassan, na madiwani wa kata zote kupitia Chama Cha Mapinduzi.