Mratibu wa mauzo kutoka kampuni ya Bonite bottles Ltd, Joseph Simplis akizungumza kwenye hafla hiyo jijini Arusha
…………..
Happy Lazaro, Arusha
Kampuni ya Bonite Bottles Ltd
wazalishaji na wasambazaji wa soda za Coca-Cola na jamii yake na maji ya Kilimanjaro wamekabithi miti 500 yenye thamani ya zaidi ya shs 3 milioni kwa shule ya Arusha sekondari ikiwa ni kampeni yake ya kupanda miti kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha shuleni hapo katika zoezi hilo la upandaji miti,Mratibu wa mauzo kutoka kampuni ya Bonite bottles Ltd, Joseph Simplis amesema shule hiyo imekabithiwa jumla ya miti 500 ambapo miti 300 ni ya matunda na miti 200 ni ya kivuli.
Simplis amesema kuwa ,lengo la kuchagua shule hii ni kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo na jinsi mahitaji ya matunda na kivuli yalivyo makubwa.
Ameongeza kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikifanya zoezi la kutunza na kuhifadhi mazingira kwa muda mrefu tangu ilipoanza 1987 ambapo mwanzilishi wake ni Dokta Hayati Reginald Mengi alikuwa ni mpenzi wa mazingira na alihakikisha kuwa mazingira yanakuwa mazuri kila mahali,hivyo hawana muda kuendeleza juhudi hizo .
Ameongeza kuwa kwa vipindi mfululizo kampuni imekuwa linashirikiana na serikali na taasisi mbalimbali katika zoezi la kuhifadhi na kutunza mazingira.
“Kwa miongo sasa zoezi hilo la kupanda miti limefanyika na mashindano mbalimbali ya kushindanisha watu kutokana na kutunza mazingira yalifanyika na kuna washindi ambao walizawadiwa kwa vipindi tofauti tofauti .”amesema Simplis .
“Jambo kubwa ambalo tunalihitaji kwa shule hii ya Arusha sekondari ni kuhakikisha kuwa miti hii inatunzwa ikue ambayo itawafaa kwa matunda ambayo ni lishe pamoja na kivuli .”
Ameongeza kuwa kwa hali ilivyo kwa wakati huu kutokana na mazingira yalivyo hamna sehemu kabisa ya kujihifadhi wakati wa jua kali hivyo tunategemea kuwa baada ya muda mchche kutakuwa na kivuli cha kutosha wanafunzi watakaohitaji kukaa chini ya kivuli au mti watakaa bila matatizo .
“Naishukuru sana jamii ya Arusha sekondari kwa jinsi ambavyo wameitikia na kuwa na furaha wafanyakazi pamoja na wanafunzi.”amesema Simplis.
Mkuu wa shule hiyo,Lorna Mtelesi amesema kuwa wamefurahi sana kwa huo upendeleo kutoka kampuni hiyo ya Bonite bottles Ltd kwa kuwapatia hiyo miti ya matunda na kivuli ambapo mingine itatumika kufundishia na kujifunzia .
“Tunawashukuru sana kampuni hii kwani tunapopokea miti tunapokea zawadi ya uhai na miti hii kwetu ni bahati kwani kwenye eneo letu kuna eneo ambalo hakuna miti.”amesema
“Miti hii itatoa kivuli wakati wa michezo matunda kwa ajili ya afya tushukuru sana kwa ajili ya miti hii na oxygen ambayo tunashukuru sana kampuni hii kwani imetusaidia sana kutokana na ukame uliokuwepo kwenye eneo hilo “amesema.
Amesema kuwa ,tunawashukuru Bonite kwa ajili ya huduma zingine kama maji na tunashukuru sana kwa sapoti yao wanaendelea kutoa kwenye mashule kwani wanatusaidia sana.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule hiyo Innocent Karao mwanafunzi wa kidato cha sita amesema kuwa ,anashukuru sana kampuni hiyo kwa namna ilivyowasaidia kwa kuona maeneo haya yalikuwa yanakosa miti kwani jua lilikuwa linawaathiri sana hususani majira ya kujisomea kwa sababu ya jua .
Amesema kuwa wanapopata miti kama hii wanapata sehemu nzuri ya kujisomea kwa utulivu na inasaidia sana kwani inaepusha magonjwa mengine ambayo yangeweza kutokea na kuepukana na magonjwa mbalimbali .
Naye Lilian Shirima mwanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapo amesema kuwa anashukuru sana kwa kampuni hiyo kuwasaidia miti kwani kwa muda mrefu walikuwa na upungufu wa miti ya kivuli hivyo kupitia miti hii waliyopanda watapata vivuli vya kutosha na mazingira rafiki ya kujifunzia ,matunda ya kutosha pia .
“Kupitia miti hiyo tunaweza kupata mvua za kutosha matunda vivuli ambavyo vitakuwa ni njianl sahihi ya kufaulu katika mitihani yao wameahidi kutunza vizuri miti hiyo kwa faida yao na wadogo zao wanaokuja.”amesema.



