
Kupitia Kipindi cha The Hard Talk kinachoongozwa na mtangazaji, mwandishi wa vitabu na mtumishi wa Mungu, @lillianmwasha_ , mwanadada Grace Tarimo amefunguka kuhusu tatizo kubwa linalomsumbua kwenye maisha yake.
Grace anajishughulisha na kazi ya kufanya ‘masaji’ kwenye saluni lakini kubwa zaidi, analo tatizo la kujichua ambalo mwenyewe ameeleza kuwa lilianza kumsumbua tangu akiwa darasa la tano.
Kwa huzuni, ameeleza kuwa kazi anayofanya imefanya tatizo hilo lizidi kuwa baya zaidi kiasi cha kumfanya apoteze dira katika kila kitu anachokifanya maishani.