Na Meleka Kulwa -Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule, amesema kuwa lengo la kikao na wamiliki wa hoteli Mkoa Wa Dodoma ni kuwaeleza miradi iliyotekelezwa na serikali katika Jiji la Dodoma, huku akibainisha kuwa serikali na sekta binafsi zinafanya kazi kwa kutegemeana.
”Tunatarajia mliyoyaona yatawapengezea shauku ya uwekezaji kwa sababu kwa upande wa serikali miundombinu imewekwa na serikali imefanya kazi kubwa sana, iliyobaki ni upande wa sekta binafsi,” amesema Bi. Senyamule.
Amesema hayo Septemba 30, 2025 jijini Dodoma, alipokutana na wamiliki wa hoteli wa Mkoa wa Dodoma.
Aidha, amebainisha kuwa serikali bado inadhamira ya kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha mikutano na utalii, huku akibainisha kuwa sekta ya wafanyabiashara wa hoteli ni muhimu sana.
Bi. Senyamule amesema kuwa kukosekana kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano kumekuwa kikwazo kwa mikutano mikubwa ya kimataifa kufanyika jijini humo licha ya uwepo wa makao makuu ya serikali.
”Hivi sasa hatuna hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo zingeweza kutumiwa na wageni wa kimataifa. Siku moja alikuja mgeni mmoja hapa Dodoma akasema hawezi kulala hapa kwa kuwa hakuna hoteli yenye hadhi ya nyota tano, ikamlazimu asafiri kwenda nje ya Dodoma ili apate eneo la kulala,” amesema
Aidha, amesema kuwa viwango vya kimataifa vinahitaji kuwepo kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano zisizopungua tano ili kuruhusu kufanyika kwa mikutano mikubwa ya kimataifa katika eneo husika.
”Nitoe wito kwa wawekezaji kuwekeza hoteli zenye hadhi ya nyota tano au mziboreshe zilizopo hivi sasa ili ziweze kufikia hadhi hiyo, kwa kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana ikiwamo ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato,” amesema Bi. Senyamule.
Aidha, amesema kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Mkoa wa Dodoma, hivyo ipo haja ya kutumia fursa hiyo kuwekeza kwenye hoteli kubwa zenye hadhi.
”Mikutano mikubwa ya kimataifa hua inafanyika katika makao makuu ya nchi, lakini hivi sasa hatuwezi kutokana na kukosa hoteli zenye hadhi hiyo, hivyo hatuna budi kuwekeza katika sekta hiyo,” amesema.
Pia, Bi. Senyamule ametoa wito kwa wafanyabiashara, wafanyakazi, famil

Pia, Bi. Senyamule ametoa wito kwa wafanyabiashara, wafanyakazi, familia na wageni wanaofika kulala katika hoteli hizo ifikapo Oktoba 29, waende wakapige kura.
Aidha, amesema kuwa mtu yoyote anaweza kupiga kura katika kituo chochote, ili kumchagua Rais anayemwona anamfaa.