

Mounir Nasraou Baba wa nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, ametoa jibu kali kwa wakosoaji waliokuwa wakimkosoa kuhusu mtindo wake wa maisha wa kifahari, akithibitisha kuwa anajivunia kutumia pesa za mwanawe. Katika kauli iliyosambaa mtandaoni, baba huyo alisema kwa dhahiri:
“Asante, Lamine, mwanangu. Nitatawala kwa maisha yangu yote kwa ajili yako.”
Wengi waliokuwa wakimkosoa walisema baba huyo anaishi maisha ya kifahari kwa kutumia fedha zinazotokana na mkataba na zawadi za mwanawe. Hata hivyo, kauli yake imeonyesha kuwa ni ushirikiano wa kifamilia na kwamba anajivunia mafanikio ya mwanawe na kushiriki naye furaha.

Lamine Yamal, ambaye ni mmoja wa wachezaji wachanga wenye vipaji vikubwa barani Ulaya, amekuwa akivutiwa sana na mashabiki kwa uwezo wake wa kipekee uwanjani, huku familia yake ikipata umaarufu mkubwa pia kutokana na mafanikio yake.
Kauli ya baba yake sasa imeibua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakiunga mkono na wengine wakibishana kuhusu maisha ya kifahari ya familia za wachezaji wakubwa ulaya.
Kwa sasa, baba wa Yamal amependelea kuonyesha kuwa furaha ya familia ni muhimu zaidi ya lawama za watu. Mashabiki sasa wanashangaa ni hatua gani za kifamilia zitafuata baada ya kauli hii isiyokuwa na shaka.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.