Wasafiri wa ndege nchini Tanzania sasa wanaweza kufurahia urahisi wa kulipia tiketi zao kupitia simu za mkononi, kufuatia makubaliano kati ya Shirika la Ndege la Dubai flydubai na Kampuni ya Network. Ushirikiano huu utarahisisha malipo ya tiketi kwa wateja huku ukikuza zaidi matumizi ya malipo ya simu nchini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Tanzania inakuwa nchi ya tatu katika kanda kuunganishwa na huduma hii, baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini Kenya na Uganda. Hii ni hatua muhimu katika kusukuma mbele matumizi ya malipo ya kidijitali Afrika Mashariki.
Wateja wa flydubai waliopo Tanzania sasa wanaweza kulipia safari zao kwa kutumia huduma za simu kama Mixx by Yass na Airtel Money, wanapokata tiketi moja kwa moja mtandaoni au kupitia programu ya simu ya flydubai. Huduma hii inaleta suluhisho kwa wasafiri wa Kitanzania ambao wamekuwa wakihitaji njia za malipo za ndani, salama na zisizohusisha pesa taslimu.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Bi. Judy Waruiru, Mkurugenzi Mtendaji wa Network Kanda ya Afrika Mashariki, alisema: “Ushirikiano huu unawarahisishia wateja wa flydubai kufanya malipo kwa usalama na gharama nafuu kwa njia ya simu, sambamba na njia za malipo za kadi zilizokuwepo.
Katika kipindi hiki ambapo malipo ya simu yanaendelea kukua kwa kasi, hasa Afrika Mashariki, tunajivunia kuwa mstari wa mbele katika kurahisisha huduma na kuendeleza ubunifu.”
Kwa upande wake, Bw. Sudhir Sreedharan, Makamu wa Rais wa Kitengo cha Uendeshaji Biashara (Falme za Kiarabu, GCC, Afrika na Asia Kusini) wa flydubai, aliongeza: “Ushirikiano wetu na Kampuni ya Network International unatokana na mafanikio tuliyoyashuhudia Kenya na Uganda, yakionesha dhamira yetu ya kutoa njia nyingi na rahisi za malipo kwa wateja wetu. Tunatarajia kuendelea kuhamasisha matumizi ya mifumo ya malipo ya ndani, huku tukiendeleza huduma bora za usafiri kwa wateja wetu kote duniani.” Ongezeko la matumizi ya huduma za simu
Kwa mujibu wa ripoti za karibuni za GSMA, Tanzania imejipambanua kama moja ya masoko yenye mafanikio makubwa katika huduma za fedha kwa njia ya simu barani Afrika. Kati ya mwaka 2019 na 2023, idadi ya namba za simu zilizosajiliwa kwa huduma za kifedha iliongezeka kutoka milioni 26 hadi milioni 53, huku kiwango cha matumizi kikiongezeka Classification – Internal Usekutoka asilimia 46 hadi 83%.
Katika kipindi hicho hicho, thamani ya miamala iliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 3 hadi bilioni 5.3 kwa mwaka. Takwimu hizi zinaonesha nafasi kubwa inayochukuliwa na malipo ya simu katika kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuchochea ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania.
Kuhusu flydubai imeunda mtandao mpana wenye vituo zaidi ya 135 katika nchi 57 barani Afrika, Asia na Ulaya. Shirika hili linaendelea kutoa huduma bora za usafiri wa abiria na mizigo kimataifa kwa kutumia ndege mpya 93 za kisasa aina ya Boeing 737.