Katikati ni kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mbuluma
Nyuma ni jengo la shule ya sekondari Mbuluma iliyowekewa jiwe la msingi
Na Neema Mtuka
Rukwa :Wananchi wa Kijiji cha Mbuluma kata ya Mbuluma wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa wamesema kuzinduliwa kwa shule ya sekondari ya Mbuluma sekondari kutapunguza mimba na ndoa za utotoni.
Akizungumza leo Septemba 30, 2025 mkazi wa kata ya Mbuluma Rafael Fataki amesema wanafunzi walikuwa wakitembea umbali mrefu wa kilomita 20 kwenda shule jambo lililokuwa likihatarisha maisha yao
“Kutokana na hali hiyo ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wengi walikata tamaa na kushindwa kumaliza masomo yao.”amesema Fataki.
Magreth Nzyungu mkazi wa Mbuluma amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo kutawasaidia wanafunzi kusoma kwa bidii na katika mazingira mazuri.
Wananchi hao wamesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza mimba,utoro na kuchelewa kwa wanafunzi ambao walikuwa wakisoma kata jirani ya msanzi.
Mradi wa shule hiyo ulianza na nguvu za wananchi ambapo baadae serikali ilitoa kiasi cha zaidi ya sh mill 5.8 fedha iliyotumika hadi kukamilika kwa mradi huo.
Ambapo kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanaondokana na changamoto zinazoweza kutatulika.
Ussi amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Mbuluma wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Aidha Ussi amekagua na kuweka jiwe la msingi daraja la mao ambalo lilikuwa linahatarisha maisha ya wakazi wa kata ya Mbuluma.
Wakazi hao akiwemo Sabuja Mwembeni amesema kukamilika kwa daraja hilo kutapunguza vifo vilivyokuwa vinatokea hasa kipindi cha masika na litarahisisha mawasiliano na kuifungua wilaya ya Kalambo kibiashara kwa kuwa watasafiri na kusafirisha bidhaa mbalimbali.
Mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha sh 637,566,028 ikiwa 583,180,028 ni fedha za SEQUIP ,50,900,000 ni fedha za halmashauri na 3,486,000 ni nguvu za wananchi na mpaka sasa kiasi cha sh 586,666,028 kimeshatumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Ujenzi huo ulianza kutekelezwa rasmi November 7 ,2024 na ulitarajiwa kukamilika Julai 2025.
Mwenge wa uhuru bado
unaendelea na mbio zake katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ambapo miradi mbalimbali inakaguliwa,kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa.