
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi zilizopatikana baada ya kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (OFFICE MANAGEMENT SECRETARY) – NAFASI 03
1.1 KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni, kusikiliza shida zao na kuwaelekeza sehemu husika.
- Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, vikao na safari za Mkuu wake.
- Kutafuta na kusambaza majalada/nyaraka kwenye Idara au Kitengo husika.
- Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada/nyaraka sehemu husika.
- Kupanga dondoo na kuandaa maandalizi ya vikao.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amehitimu Kidato cha Nne au Sita.
- Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.
- Awe amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika.
- Awe amepata mafunzo ya Kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.
2.0 MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 hadi 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na kuainisha aina ya ulemavu.
- Waombaji waambatishe CV yenye maelezo binafsi, mawasiliano, email, namba za simu na majina ya wadhamini watatu.
- Vyeti vyote vya elimu na taaluma viwe vimeidhinishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Testimonials, Statement of Results, Provisional Results na Slips hazitakubalika.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA, TCU au NACTVET.
- Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waajiriwa wa kada za kuingilia hawaruhusiwi kuomba kulingana na Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30/11/2010.
- Taarifa za kughushi zitasababisha hatua za kisheria.
- Waombaji wenye majina yanayotofautiana na nyaraka zao lazima wawasilishe Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll).
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Oktoba, 2025.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Oktoba, 2025
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
S.L.P 28001,
KISARAWE
FUNGUA HAPA KUOMA ZAIDI >>> TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE