Na Hamis Dambaya, Nairobi Kenya.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii duniani katika maonesho ya Magical 2025 yanayoendelea nchini Kenya wengi wakivitiwa na habari za vivutio vya utalii vilivyoko Ngorongoro na kuinyesha dhamira ya kutembelea hifadhi hiyo.
Afisa Utalii na Masoko Mkuu wa Mamlaka hiyo Michael Makombe amewaeleza wadau hao kuwa hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa kivutio bora cha utalii baranı Afrika kutokana na weledi wake wa kusimamia uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii.
“Tumefarijika kuona katika maonesho haya wageni ambao hawajafika Ngorongoro wametamani kufika,lakini tumewatembelea katika mabanda yao na kuwaeleza vivutio vyetu tulivyo navyo na wengi wameonesha nia ya kufika Ngorongoro,”alisema Makombe.
Maonesho hayo yanahusisha wadau wa sekta ya utalii kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo pamoja na kuonesha shughuli zao wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu katika sekta hiyo.