Na Meleka Kulwa -Dodoma
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI , ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa, amesema kuwa ni wajibu wa waajiri kuhakikisha watumishi wapya na waliopo kazini wanapatiwa mafunzo ya maadili ili kuimarisha uadilifu na kupunguza mianya ya rushwa katika utumishi wa umma.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, alipokuwa akifungua kikao kazi cha sita cha wadau wa usimamizi wa maadili ya kitaaluma na utendaji kilichofanyika Oktoba 2, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, jijini Dodoma.
Bi. Hilda Kabissa amesema kuwa mafunzo hayo bado hayajapewa kipaumbele katika baadhi ya ofisi za Mikoa na halmashauri, hali inayosababisha fedha zilizotengwa kwa ajili hiyo kutumika kinyume na malengo.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma, jambo lililochangia nchi kupanda kutoka nafasi ya 87 mwaka 2023 hadi nafasi ya 82 mwaka 2024 katika tathmini ya Shirika la Transparency International.
Pia, amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na kupungua kwa mianya ya rushwa katika utoaji wa huduma pamoja na juhudi za Rais Samia kuhimiza uwajibikaji na maadili, hatua inayoongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Aidha, Bi. Hilda ametoa maelekezo kwa washiriki wa kikao hicho, amesema kuwa “ni lazima uwajibikaji, matumizi sahihi ya fedha za mafunzo, uwekezaji kwenye mifumo ya TEHAMA ili kuongeza uwazi na ufanisi, pamoja na utekelezaji wa maazimio na mpangokazi unaopangwa kupitia vikao kazi” amesema
Pia, amebainisha kuwa changamoto zinazojitokeza zinapaswa kutafutiwa suluhu kwa pamoja. Aidha, amesema kuwa kikao kinachofuata kitafanyika mwezi Machi 2026 chini ya uratibu wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT)., Bi. Hilda Kabissa
amesema kuwa “Ofisi yangu kama mratibu wa vikao hivi, ifanye mawasiliano na NAOT mapema iwezekanavyo, ili kutoa nafasi ya kufanya maandalizi ya kutosha kulingana na mahitaji ya vikao hivi” amesema
Pia, Bi. Hilda amewataka watumishi wa Umma wote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni Taratibu na Mienendo ya Maadili ya Utendaji na Maadili ya Taaluma zao katika utendaji wao wa kazi, ili kutoa huduma bora kwa kuzingatia weledi, uadilifu na uwajibikaji wa hiari, kwa lengo la kuimarisha ustawi kwa wananchi, na hivyo kupunguza malalamiko ya wananchi na kuwaongezea imani kwa serikali yao.
“Aidha, Bi. Hilda Kabissa ametoa wito kwa wananchi kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025, akisema kuwa “mjitokeze kwenye vituo mliyojiandikishia na kuchagua viongozi wenu ili kuendeleza amani na maendeleo” amesema
Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Bi. Felister Shuli, amesema kuwa kikao kazi hicho ni matokeo ya maazimio ya kikao cha tatu kilichofanyika Septemba 2023 jijini Dodoma, ambapo iliazimiwa vikao kama hivyo vifanyike mara mbili kwa mwaka kwa mfumo wa mzunguko.
Aidha, amebainisha kuwa kikao cha tano kiliratibiwa na TAKUKURU mwezi Julai 2025 na kikao cha sasa kimeratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikao, Bw. Salvatory Kilasara kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, amesema kuwa washiriki wa kikao hicho ni pamoja na taasisi simamizi za maadili ya kitaaluma, taasisi za maadili ya utendaji na waratibu wa mafunzo