Gavana wa Anjouan katika Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Dkt. Zaidou Youssouf akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu na Madaktari Bingwa kutoka Tanzania wakiwamo wa moyo mara baada ya kukukutana na wataalamu hao leo ofisini kwake. Timu ya wataalamu wa afya kutoka Tanzania iko kisiwani Anjouan kwaajili ya kutoa huduma za ubingwa bobezi za matibabu ya magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa visiwa vya Comoro.
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Bingwa kutoka Tanzania na wataalamu wa afya wa hospitali ya Hombo iliyopo kisiwani Anjouan mara baada ya kumaliza kuangalia maeneo watakayotolea huduma za kibingwa za matibabu ya magonjwa mbalimbali zitakazotolewa katika hospitali hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akitoa neno la shukrani kwa Gavana wa kisiwa cha Anjouan katika Muungano wa Visiwa vya Comoro Dkt. Zaidou Youssouf wakati madaktari bingwa kutoka Tanzania walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi katika hospitali tatu kubwa zilizopo kisiwani humo. (Picha na JKCI)
………….