

Kocha wa Manchester United, Rúben Amorim, yuko katika hatihati ya kufutwa kazi endapo kikosi chake kitashindwa kupata ushindi dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) utakaochezwa leo jioni.
Taarifa zinasema kuwa Sir Jim Ratcliffe bado anataka kumpa Amorim nafasi ya kuendelea, lakini msimamo huo unaweza kubadilika haraka iwapo matokeo dhidi ya Sunderland hayatakuwa mazuri.
Ingawa Manchester United wanapewa nafasi kubwa ya ushindi, kipigo kingine kitazidisha shinikizo kubwa kwa Amorim, ambaye anatazamwa kama ana kazi ya kuthibitisha uwezo wake msimu huu.
Hadi sasa, Mashetani Wekundu wamepoteza mchezo mmoja pekee kati ya mitatu ya nyumbani msimu wa 2025/26, wakipata ushindi dhidi ya Burnley na Chelsea katika Uwanja wa Old Trafford.
Hata hivyo, Sunderland wanaoingia kwenye mchezo huo wakiwa katika hali nzuri ya mchezo, wameanza msimu kwa ubora mkubwa tangu kurejea kutoka Championship, na kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi pointi nne mbele ya United.
VIGOGO CHADEMA WABURUZWA MAHAKAMANI – WAMO HECHE – MNYIKA na WENGINE -KIGOGO ZANZIBAR AWAFUNGIA KAZI